
|
UTANGULIZI |
|
Mawasiliano ya kutumia lugha ni nyenzo muhimu sana inayomwezesha mwanadamu kutangamana na kuingiliana na wenzake. Watu waishio katika jamii hulazimika kuwasiliana kwa maandishi au mazungumzo ili kutimiza malengo kadha. Baadhi ya shabaha za mawasiliano ni kama vile kutimiza haja fulani kwa mfano, mahitaji ya maisha ya kila siku kama riziki, makao, usafiri, matibabu na mengineyo. Pili, mawasiliano hutuwezesha kupashana habari za aina mbalimbali na pia hutuwezesha kukusanya, kuchambua na kuhifadhi kumbukumbu muhimu. Kupitia mbinu tofauti za mawasiliano, tunaweza kuelimishana na kujipatia maarifa muhimu ya kutuwezesha kuzikabili changamoto zinazotukumba katika maisha ya kila siku. |
- Enseignant: MAGNIFIQUE IDAHEMUKA