Moduli hii inamwezesha mwanafunzi kukuza uwezo wa kutumia Kiswahili katika mawasiliano ya msingi ya kila siku, masomo na mazingira ya kazi. Mwanafunzi atajifunza kutumia msamiati unaofaa katika kujitambulisha, kutoa taarifa binafsi, kutumia namba, kiasi, tarehe na muda, pamoja na kutumia msamiati kulingana na muktadha wa mawasiliano. Aidha, moduli inajikita katika sarufi ya Kiswahili kwa kumwezesha mwanafunzi kubaini na kutumia nafsi, kubaini muundo wa vitenzi vya Kiswahili, vikiwemo vitenzi vya Kibantu, vitenzi vya kigeni na vitenzi vya silabi moja, na kutumia nyakati mbalimbali za Kiswahili kwa usahihi. Pia, mwanafunzi atajifunza istilahi mahsusi za taaluma yake na matumizi ya hati rahisi za kikazi na kibiashara katika mazingira halisi ya kazi.